Misaada ya Kujifunza
Hesabu


Hesabu

Kitabu cha nne katika Agano la Kale. Musa aliandika kitabu hiki cha Hesabu. Kitabu cha Hesabu kinaelezea hadithi ya safari ya Israeli kutoka Mlima Sinai hadi nyanda za Moabu juu ya mpaka wa Kanaani. Moja ya masomo muhimu kinacho fundisha ni kwamba watu wa Mungu lazima watembee kwa imani, wakiamini ahadi Zake, kama wanataka kuendelea kwa mafanikio. Kinaelezea adhabu za Mungu kwa Israeli kwa sababu ya utovu wa utiifu na hutoa taarifa juu ya sheria za Waisraeli. Jina la kitabu linatokana na tarakimu ya sensa maarufu (Hes. 1–2; 26).

Mlango wa 1–10 inasimulia juu ya maandilizi ya Waisraeli ya kuondoka toka Sinai. Mlango wa 11–14 inaelezea juu ya msafara wenyewe, kutumwa kwa wapelelezi ndani ya Kanaani, na kukataliwa kwa Israeli kuingia nchi ya ahadi. Mlango wa 15–19 inaonyesha sheria kadha wa kadha na matukio ya kihistoria. Mlango wa 20–36 ni historia ya mwaka wa mwisho wa watu hawa nyikani.