Misaada ya Kujifunza
Isaya


Isaya

Nabii wa Agano la Kale aliyetoa unabii tangu mwaka 740–701 K.K. Kama mshauri mkuu wa Mfalme Hezekia, Isaya alikuwa na nguvu kubwa za kidini na kisiasa.

Yesu alikuwa akimnukuu Isaya mara nyingi zaidi kuliko Alivyomnukuu nabii mwingine yeyote. Petro, Yohana, na Paulo pia mara kwa mara walimnukuu Isaya, katika Agano Jipya. Kitabu cha Mormoni na Mafundisho na Maagano vina nukuu nyingi kutoka kwa Isaya kuliko kutoka kwa nabii mwingine yeyote navyo hutoa msaada mkubwa katika kumfafanua Isaya. Nefi aliwafundisha watu wake kutoka kwenye maandiko ya Isaya (2 Ne. 12–24; Isa. 2–14). Bwana aliwaambia Wanefi ya kwamba “maneno ya Isaya ni makuu” na kwamba mambo yote aliyoyatolea unabii yangetimia (3 Ne. 23:1–3).

Kitabu cha Isaya

Kitabu katika Agano la Kale. Unabii mwingi wa Isaya unahusiana na kuja kwa Mkombozi katika huduma Yake ya duniani (Isa. 9:6) na kama Mfalme Mkuu katika siku ya mwisho (Isa. 63). Pia alitoa unabii mwingi juu ya hali ya baadaye ya Israeli.

Mlango wa 1 ni utangulizi wa kitabu chote. Isaya 7:14; 9:6–7; 11:1–5; 53; na 61:1–3 zinaonyesha misheni ya Mwokozi. Mlango wa 2, 11, 12, na 35 hujishughulisha na matukio katika siku za mwisho, wakati injili itakaporejeshwa, Israeli itakusanywa, na nchi yenye kiu itakapochanua kama ua la waridi. Mlango wa 29 ina unabii wa ujio wa Kitabu cha Mormoni (2 Ne. 27). Mlango wa 40–46 inatangaza ukuu wa Yehova kama Mungu wa kweli aliye juu ya miungu sanamu waabudiwao na wapagani. Milango inayobaki 47–66, hujishughulisha na matukio katika urejesho wa mwisho wa Israeli na kuanzishwa kwa Sayuni, pamoja na Bwana kukaa miongoni mwa watu Wake.