Misaada ya Kujifunza
Yusufu, Mwana wa Yakobo


Yusufu, Mwana wa Yakobo

Katika Agano la Kale, ni mwana mzaliwa wa kwanza wa Yakobo na Raheli (Mwa. 30:22–24; 37:3).

Yusufu alijipatia haki ya uzaliwa wa kwanza katika Israeli kwa sababu Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa mke wa kwanza wa Yakobo, alipoteza haki hii kwa uvunjaji wa sheria (1 Nya. 5:1–2). Kwa sababu alikuwa mtu mwenye kustahili, Yusufu, kama mwana mzaliwa wa kwanza wa mke wa pili wa Yakobo, alikuwa ndiye anayefuatia katika mstari kwa ajili ya baraka hiyo. Yusufu pia alipokea baraka kutoka kwa baba yake muda mfupi tu kabla ya Yakobo kufa (Mwa. 49:22–26).

Yusufu alikuwa mtu mwadilifu sana “mwangalifu na mwenye hekima” (Mwa. 41:39). Kumkatalia kwake mke wa Potifa ni mfano wa imani, usafi wa kimwili, na uadilifu wa kibinafsi (Mwa. 39:7–12). Katika Misri, wakati Yusufu alipofunua utambulisho wake wa kweli kwa kaka zake, aliwashukuru badala ya kuwashutumu kwa jinsi walivyomtendea yeye. Aliamini matendo yao yamesaidia kutimiza mapenzi matakatifu ya Mungu (Mwa. 45:4–15).

Ufunuo wa siku za mwisho unafunua huduma ya familia ya Yusufu katika siku za mwisho (TJS, Mwa. 50:24–38 [Kiambatisho]; 2 Ne. 3:3–24; 3 Ne. 20:25–27).