Misaada ya Kujifunza
Paulo


Paulo

Mtume katika Agano Jipya. Jina la Paulo la Kiebrania lilikuwa ni Sauli, na alikuwa akijulikana kwa jina hili hadi kuanza kwa misheni yake kwa Wayunani. Mwanzoni alilitesa Kanisa hadi alipoongolewa katika ukweli wake baada ya kuona ono la Yesu Kristo. Paulo alienda katika safari kuu tatu za kimisionari na aliandika barua nyingi kwa Watakatifu. Kumi na nne kati ya barua hizi zimeunda sehemu ya Agano Jipya siku hizi. Hatimaye alichukuliwa kama mfungwa hadi Roma na akauawa, huenda katika majira ya kuchipua ya mwaka 65 B.K.