Misaada ya Kujifunza
Msalaba


Msalaba

Umbile la kitu kilichotengenezwa kwa mbao ambapo juu yake Yesu Kristo alisulubiwa (Mk. 15:20–26). Wengi duniani sasa wanaifikiria hiyo kama ndiyo alama ya Kusulubiwa kwa Kristo na dhabihu ya kulipia dhambi; hata hivyo, Bwana ameweka alama Zake mwenyewe kwa ajili ya Kusulubiwa Kwake na dhabihu Yake—mkate na maji ya sakramenti (Mt. 26:26–28; M&M 20:40, 75–79). Katika maandiko, wale wachukuao msalaba wao ni wale wenye kumpenda Yesu Kristo sana kiasi kwamba hukataa ubaya na tamaa za kidunia na kushika amri Zake (TJS, Mt. 16:25–26 [Kiambatisho]).