Misaada ya Kujifunza
Timotheo


Timotheo

Katika Agano Jipya, ni mmsionari kijana mshirika wa Paulo wakati wa huduma za Paulo (Mdo. 16:1–3; 2 Tim. 1:1–5); mwana wa baba Myunani na mama Myahudi; yeye na wazazi wake waliishi katika Listra.

Paulo alizungumza juu ya Timotheo kama “mwanawe hasa katika imani” (1 Tim. 1:2, 18; 2 Tim. 1:2). Timoteo huenda alikuwa ndiye msaidizi wa Paulo aliyeaminika na mwenye uwezo zaidi (Flp. 2:19–23).