Misaada ya Kujifunza
Kumora, Mlima


Kumora, Mlima

Kilima kidogo kilichoko magharibi ya New York, Marekani. Hapa ndipo nabii wa kale aliyeitwa Moroni alipoyaficha yale mabamba ya dhahabu yaliyokuwa na maandiko ya mataifa ya Wanefi na Wayaredi. Joseph Smith alielekezwa kwenda katika kilima hiki katika mwaka 1827 na Moroni mfufuka ili kuchukua mabamba haya na kutafsiri sehemu yake. Tafsiri hii ndicho Kitabu cha Mormoni.