Misaada ya Kujifunza
Kigingi


Kigingi

Kitengo kimojawapo cha utaratibu na utawala wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kigingi kinaundwa na idadi kadhaa ya wadi au matawi. Kwa ujumla kina mipaka ya kijiografia iliyowekwa na inafanana na taswira ya hema inayoelezewa katika Isaya 54:2: “Refusha kamba zako na kuimarisha vigingi vyako.” Kila kigingi cha Sayuni kinahimili na kusaidia kushikia Kanisa kwa namna ambayo hema au maskani linavyoshikiliwa na vigingi. Kigingi ni mahali pa kukusanyikia kwa ajili ya mabaki ya Israeli waliotawanywa (M&M 82:13–14; 101:17–21).